ELCT North Eastern Diocese
Ziari ya Askofu Mteule Mch.Dkt.Msafiri Joseph Mbilu na Kaimu Katibu Mkuu Mission ya Kigoma
- Details
Askofu Mteule Mch. Dkt. Msafiri J. Mbilu yupo ziarani katika Mission ya Kigoma ambapo ameshiriki katika kikao cha maandalizi ya Mission hiyo inayoandaliwa kuwa Dayosisi.
Askofu Andrew Petrol Gulle na Katibu Mkuu Bw. Rigath Mille wa KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria na Askofu Dkt.Abednego N. Keshomshahara na Katibu Mkuu Mch. Elimerek Kigembe wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Magharibi pia wameshiriki katika kikao hicho.
Ikumbukwe Mission hii ya Kigoma inatunzwa na KKK-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Magharibi (Bukoba) na KKKT- Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria.
Pamoja na hayo Askofu Mteule Mch.Dkt Mbilu ambaye ameambatana na kaimu Katibu Mkuu Mch.Godfrey Walalaze amepata nafasi ya kutembelea Mitaa na Sharikia za Mission hiyo ambapo amejionea miradi na kazi mbalimbali zinazo fanywa ndani ya mission hiyo.
Askofu Mteule Mch. Dkt. Mbilu amemshukuru Mch. Lazaro Rohho Mratibu wa Mission pamoja na waumini wa Mission hiyo kwa mapokezi mazuri, ambapo katika itikio lake juu ya mahitaji mbambali yaliyo wekwa mbele yake, Askofu Mch.Dkt Mbilu ameahidi kutoa ushirikiano na kusaidiana katika kazi mbalimbali zinazoendelea. Pia aliwaasa Wakristo wa Missioni kujifunga katika kifungo cha Umoja na kuruhusu Mungu awafundishe, awaongoze na kuwashauri katika kila hatua kuelekea kuzaliwa kwa Dayosisi mpya.
- Hits: 484
Wahitimu wa mafunzo ya Muziki Kanisa Kuu Lushoto
- Details
Wahitimu wa Muziki (Tarumbeta) wakiwa katika picha ya pamoja na mwalimu wao ndugu Michael Kivulenge wa kwanza kutoka kulia mara baada ya Ibada Kanisa Kuu Lushoto. Leo tarehe 21/02/2021
- Hits: 483
Hatimaye mwili wa aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SEKOMU Prof. Kihiyo waagwa rasmi.
- Details
Picha za matukio mbalimbali ya kuaga mwili wa aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Prof. Vincent Kihiyo,Katika ukumbi wa mihadhara Sekomu na Nyumbani kwa Marehemu.
- Hits: 645
Page 1 of 28