ELCT North Eastern Diocese
Askofu Mteule wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, aeendelea kutambulishwa
- Details
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, leo ameendelea kutambulishwa katika sharika mbalimbali za Dayosisi ambapo leo ameshiriki ibada ya Jumapili katika usharika wa Soni Jimbo la Kusini huku akiwataka waumini wa usharika huo kuanzisha miradi mbalimbali itakayowainua kiuchumi.
Askofu Mteule Mch. Dkt. Mbilu ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali wateule akiwemo msaidizi wake Mch. Michael Kanju pamoja na Kaimu Katibu Mkuu Mch. Godfrey Walalaze, amesema kuwa waumini wakiwa na miradi ambayo inawapatia kipato wataweza kushiriki vyema katika kuimarisha kazi za Dayosisi hususani katika nyanja za elimu, afya, na utumishi wa kiroho.
Sambamba na hayo Mch Dkt. Mbilu amesema kuwa Dayosisi imeamua kutoa punguzo kwa wanadayosisi watakaokwenda katika hospitali ya Bumbuli kwa ajili ya matibabu kuwa watapata punguzo la asilimia 10 ya gharama za matibabu.
Pamoja na hayo ameendelea kutoa mwaliko kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika shule zinazomilikiwa na Dayosisi ikiwemo Lwandai na Bangala kwa kuwa watapata punguzo la asilimia 10 ya karo kama ilivyo kwa Hospitali ya Bumbuli.
“Napenda kutoa mwaliko kwa wanadayosisi kuwapeleka Watoto wao kusoma katika shule zetu za Bangala na Lwandai ambapo tumekubaliana kutakuwa na punguzo la asilimia 10 ya ada ilimradi tu uwe na namba ya ahadi”, Alisema Mch. Dkt. Mbilu.
Aidha Mch. Dkt. Mbilu amesema ataendelea kusimamia uimarishaji wa mafundisho sahihi ya Neno la Mungu kwa kuwa kumekuwa na mafundisho potofu ambayo yanaleta mkanganyiko kwa waumini.
Pia Askofu Mteule amepata wasaa wa kuzindua kalenda ya Dayosisi inayoongozwa na Neno kuu la Dayosisi kutoka Zaburi 32:8 “Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
Today the 17th of January, Bishop Elect Rev. Dr. Msafiri Mbilu led a worship service at Soni Parish (the head quarters of the Southern Superintendent) where he was introduced to the congregants.
In his speech, Bishop Elect Rev. Dr. Mbilu asserted that he, his Assistant, Acting General Secretary, members of the Executive Council of the Diocese and Superintendents of our respective Districts wholeheartedly accepted the responsibilities of serving God in this Diocese.
Explaining how they were committed to revamp various dormant works in the Diocese, Bishop Elect said that there were special discounts (10%) in our secondary schools and Bumbuli Hospital for all parishioners in the Diocese for respective services offered.
Talking about teachings of faith in the Diocese, Bishop Elect underscored His commitment to overseeing sound Lutheran Christian Doctrines since there is currently a wave of pervasive teachings in the Diocese and elsewhere.
- Hits: 134
Askofu Mteule Mch. Dr. Msafiri Mbilu na viongozi wengine wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki wamtembelea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Dodoma.
- Details
Askofu Mteule Mch. Dr. Msafiri Mbilu na viongozi wengine wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki pamoja na uongozi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa SEKOMU wamemtembelea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa .
Ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameutaka uongozi mpya wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ambao ndio wamiliki wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) ukamilishe mahitaji ambayo yataiwezesha Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kukiruhusu chuo hicho kuendelea na udahili.
Mhe. Kassim Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, Januari 16, 2021 wakati alipokutana na Askofu Mteule Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ambaye aliambatana na viongozi wengine wa Dayosisi. Kikao kimefanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa Dododoma.
Dean Mteule wa KKKT-DKMS,Mch. Michael Kanju akisalimiana na WAZIRI MKUU waTanzania,Mhe.Kassim Majaliwa
Kaimu Katibu Mkuu wa KKKT-DKMS Mch. Godfrey Walalaze akisalimiana na WAZIRI MKUU waTanzania, Mhe.Kassim Majaliwa
Mkuu wa Jimbo Mteule wa jimbo la Pwani Mch. Thadeus Ketto akisalimiana na WAZIRI MKUU waTanzania, Mhe.Kassim Majaliwa
Mkuu wa Jimbo Mteule wa jimbo la Kaskazini Mch.Anderson Kipande, akisalimiana na WAZIRI MKUU waTanzania,Mhe. Kassim Majaliwa
Mkuu wa Jimbo Mteule wa jimbo la Tambarare Mch. Frank Mtangi, akisalimiana na WAZIRI MKUU waTanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SEKOMU Prof. Vincent Kihiyo, akisalimiana na WAZIRI MKUU wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango,Fedha na Utawala Prof. Joseph Mbatia akisalimiana na WAZIRI MKUU wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
Mhe. Kassim Majaliwa, ametumia fulsa hiyo kuwashukuru viongozi wa Dini Nchini kwa mchango mkubwa kwa Taifa ambapo amesema "Viongozi wa Dini ni watu muhimu sana, Inchi imetulia na ina amani , hivyo kuwa kimbilio kwa waliokosa amani makwao"
- Hits: 381
Kikao cha Baba Askofu Jimbo la Pwani
- Details
Leo tarehe 10/01/2021 Askofu Mteule Mch Dkt Msafiri Joseph Mbilu mara baada ya Ibada katika Usharika wa Kana Jimbo la Pwani,amepata nafasi ya kufanya kikao na baadhi ya wazee wa Kanisa na Wazee maarufu wa Jimbo la Pwani. Kikao kilifanyika katika hostel ya Mbuyu Kenda Tanga lengo likiwa ni kupata maoni ya wazee hao juu ya namna bora ya kuiendeleza na kuiimarisha hostel ya Mbuyukenda.
- Hits: 238
Kikao cha tathmini ya kazi za Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMS)
- Details
Kikao cha tathmini ya kazi za Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMS) ambacho kimeanza kufanyika leo hii tarehe 6-9/01/2021 kimefunguliwa na Dean Mteule Mch Michael Kanju kwa niaba ya Askofu Mteule Mch Msafiri Joseph Mbilu ambaye katika utangulizi wa semina hii alisoma neno kuu la mwaka KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kutoka kitabu cha Zaburi: 32:8 “Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;Nitakushauri, Jicho langu likikutazama”.
Malengo ya kikao hiki ni kuweka vipaombele vya Dayosisi kwa mwaka 2021
- Hits: 490
Page 1 of 25