Chuo cha Utabibu cha Bumbuli, Bumbuli Clinical Officer’s Training Center (COTC), kinapenda kuwatangazia wahitimu wote wa Kidato cha Nne (4) na wanaotaka kujiendeleza na masomo yao yaani Upgrading kuwa nafasi za masomo sasa zipo wazi mpaka ifikapo tarehe 20/02/2020.

 

Chuo kina mazingira tulivu na mazuri ya kujisomea, Maktaba nzuri, Maabara ya kisasa na chuo chetu kina walimu wazuri waliobobea na kukubalika na NACTE.

Chuo kinapatika Mkoa wa Tanga, Wilaya ya Lushoto, Halmashauri ya Bumbuli.

Chuo kinatoa kozi zifuatazo:

  1. Stashaada ya Utabibu kwa wanafunzi wanaoanza ( Diploma in clinical medicine Direct Entry): Mwanafunzi anapaswa kuwa na ufaulu wa kuanzia D katika masomo yake ya Fisikia (Physics) , Kemia (Chemistry) na baiologia (Biology), ufaulu wa somo la Hesabu na kiingereza hautafuatiliwa ila utapewa kipaumbele pale itakapotokea nafasi ni chache.

 

  1. Stashaada ya utabibu kwa wanafunzi wanaotaka kujiendeleza (Diploma in Clinical Medicine Upgrading): Mwanafunzi anapaswa kuwa na ufaulu wa kuanzia GPA 2.0 katika ngazi ya cheti ya kozi ya utabibu yaani NTA Level 5, pia anatakiwa kuambatanisha vyeti vyake vyote ya cheti ya NTA level 5, Cheti cha kidato cha Nne (4) na Cheti cha Kuzaliwa.

Ili kuweza kufanya maombi mtandaoni tafadhali pitia link hii hapa : https://www.bumbulicotc.ac.tz/enroll

Kwa mawasiliano Zaidi wasiliana nasi kupitia namba : 0625867170, 0767674380, 0768003811 au 0752778535