Tarehe 13/09/2020 ilikuwa siku ya furaha katika Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dinari ya Tambarare ambapo tulikuwa na uzinduzi wa Usharika mpya ambao umepewa hadhi ya kuwa usharika kamili na unatambulika kwa jina la Usharika wa Eden Kilindi Asilia.
 
Ibada hiyo iliongozwa na Baba Dean Dkt Eberhardt Ngugi akishirikiana na Mch Yambazi Mauya Mkuu wa Dinari ya Tambarare. Usharika wa Eden Kilindi Asilia unaongozwa na Mch Benson S. Kimweri.
Ibada ilihudhuriwa na Katibu Mkuu Mch James Mwinuka, Wachungaji, Wainjilisti, Mashemasi, Kwaya, Washarika pamoja na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Usharika wa Eden Kilindi Asilia.

 The inauguration of the parish of Eden Kilindi Asilia in the plain Deanery of the North Eastern Diocese. The name comes from the area of Kilindi Asilia where the parish is located. Currently the pastor managing this parish is Rev Benson Kimweri.

 This event took place on Sunday 13th of September 2020 whereby those who attended were Rev Dr Eberhardt Ngugi who led the service, and was assisted in the liturgy by Rev Yambazi Mauya is the Dean from the plain Deanery. Others were Rev James Mwinuka NED General Secretary, pastors, evangelists, deacons, choirs and church members from within and outside the parish.