Msaidizi wa  Askofu ,Mch. Michael Kanju ambaye aliambatana na Mratibu wa Misioni na Uinjilisti Mch John Ndimbo. wamepata nafasi ya kumpokea Mwl. Christopher Mwakasege ambaye hapo kesho atapata nafasi ya kushiriki na kufundisha Neno la Mungu katika Mkutano wa wachungaji ulioanza leo tarehe 10/02/2021

uliofunguliwa na Mhe. Askofu mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Dkt. Msafiri Mbilu katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa SEKOMU.

Ikumbukwe Mwl. Christopher Mwakasege atapata nafasi ya kufundisha neno la Mungu katika semina itakayofanyika siku ya Ijumaa tarehe 12/02/2021 Kanisa Kuu Lushoto Cathedral.