TANGAZO  MKUU WA CHUO  CHA TANGA TECHNICAL INSTITUTE (TTI) KINACHOMILIKIWA NA DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI KKKT

ANAKARIBISHA MAOMBI YA KUJIUNGA NA CHUO MWEZI MACHI ( MARCH INTAKE), 2020.

CHUO KIPO JIJINI TANGA, MKABALA NA SOKO LA TANGAMANO, NYUMA YA KANISA LA KKKT  KANA (BARABARA YA NANE).

 

KOZI ZINATOLEWA KATIKA FANI ZIFUATAZO

 A.KOZI ZA ASTASHAHADA (BASIC CERTIFICATE)

1. ASTASHAHADA YA UONGOZI WA BIASHARA (BASIC CERTIFICATE IN   BUSINESS ADMINISTRATION) 

Sifa za kujiunga:

Alama  za ufaulu katika kiwango cha D nne (4) au zaidi za Kidato cha Nne kwa masomo ambayo siyo ya dini. Kati ya  hizo D nne ( 4 ) mojawapo iwe ni ya  Hisabati.

 2. ASTASHAHADA YA UHASIBU NA FEDHA (BASIC CERTIFICATE IN ACCOUNTING AND FINANCE)

Sifa za Kujiunga:

Alama  za ufaulu katika kiwango cha D nne (4) au zaidi za Kidato cha Nne kwa masomo ambayo siyo ya dini. Kati ya hizo D nne (4) mojawapo iwe ni ya Hisabati, Commerce au Book-keeping.

 B. KOZI ZA STASHAHADA (DIPLOMA)

 

  1. STASHAHADA YA UONGOZI WA BIASHARA (DIPLOMA IN BUSINESS  ADMINISTRATION) 

Sifa za kujiunga:

  1. Astashahada ya Uongozi wa Biashara yaani (Basic Certificate in Business Administration) ya ufaulu wa daraja la pili kutoka vyuo au taasisi zinazotambuliwa na NACTE.
  2. Kidato cha Sita ufaulu wa angalau alama ‘E’ moja na Subsidiary moja au angalau ‘C’ tatu za Kidato cha Nne. Mwombaji lazima awe amefaulu somo la Hisabati au Biashara kwa ufaulu angalau alama ‘D’ katika Kidato cha Nne.
  3. Kama ‘E’ ya Kidato cha Sita sio somo la Hisabati au Biashara basi mwombaji awe angalau na alama ‘C’ katika Kidato cha Nne (4) kwa somo hilo.

 

  1. STASHAHADA YA UHASIBU NA FEDHA (DIPLOMA IN ACCOUNTANCY AND FINANCE)

Sifa za kujiunga:

  1. Astashahada ya Uhasibu na Fedha (Basic Certificate in Accountancy and Finance) ya ufaulu wa daraja la pili kutoka vyuo au taasisi zinazotambuliwa na NACTE.
  2. Kidato cha Sita ufaulu wa angalau alama ‘E’ moja na Subsidiary moja au angalau ‘C’ tatu za Kidato cha Nne (4). Mwombaji lazima awe amefaulu somo la Hisabati au Biashara kwa ufaulu angalau alama ‘D’ katika Kidato cha Nne.
  3. Kama ‘E’ ya Kidato cha Sita sio somo la Hisabati au Biashara basi mwombaji awe angalau na alama ‘C’ katika Kidato cha Nne kwa somo hilo.

 

Fomu za kujiunga zinapatikana Chuoni na kwenye sharika za KKKT Kana, Makorora, Kisosora, Mikanjuni, Korogwe, Mombo, Lushoto, Kange na nyinginezo.

Kwa mawasiliano zaidi piga:

  1. Mkuu wa Chuo -0718 911 334/0689488887
  2. Msajili - 0716 444 902/0783176000