Print

Leo imekuwa  siku ya furaha na shangwe katika Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ,Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dinari ya Pwani baada kanda mbili za usharika wa Makorora kupewa hadhi ya  kuwa sharika zinazo jitegemea.

Kanda hizo ni Duga Maforoni ambapo umepewa hadhi ya kuwa usharika kamili  na unatambulika kwa jina la Usharika wa Bethlehemu, Aidha kanda ya Amboni iliyokuwa chini ya uongozi wa Usharika Mama wa Makorora  nao umepewa hadhi ya kuwa Usharika kamili na kuanzia leo unatambulika kama Usharika wa  Bethania.Ibada hiyo imeongozwa na Askofu Dkt Stephen I. Munga akishirikiana na Msaidizi wa Askofu Mch.Dkt Eberhardt Ngugi , Katibu Mkuu Mch James Mwinuka, Mkuu wa Dinari ya Pwani Mch Moses Shemweta pamoja na Wachungaji.

Usharika wa Bethlehemu unaongozwa na Mch Erasto Msumari wakati usharika wa Bethania unaongozwa na Mch Mstaafu Emannuel Mtoi.

 Awali kanda hizo zilikuwa chini ya Usharika wa Makorora zikiongozwa na Mch John Ndimbo

                                                             Mchungaji mstaafu Emmanuel Mtoi pamoja na Mke wake