MAHAFALI YA  SHULE YA MSINGI YA WASIOONA IRENTE

Leo Tarehe 20/09/2019 yamefanyika mahafali ya 47 ya darasa la saba tangu kuanzishwa kwa Shule ya Msingi ya Wasioona Irente  mwaka 1963. Katika mahafali hayo walihitimu wanafunzi wanane. Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa Baba Askofu  wa DKMs  aliyewakilishwa na Mch Paulo Diu, Mratibu Elimu wa Dayosisi, ambaye aliisihi jamii kutowatenga au kuwadharau  watu wenye mahitaji maalumu. Miongoni mwa watu waliohudhuria mahafali hayo ni pamoja na Stephen Shemdoe, Afisa Elimu Maalumu Wilaya ya Lushoto, Glory Mdemu, Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Lushoto ,Mch Happyness Diu, Mratibu wa Jinsia na Watoto, Wakuu wa vituo  vya Irente, shule jirani na wageni mbalimbali. Vilevile kulifanyika harambee ndogo ya kuchangia maendeleo ya shule hii.  Awali kabla ya kuingia ukumbini mgeni rasmi alishuhudia maonesho yaliyoandaliwa na walimu na wanafunzi wa shule hii.

 

 

 THE 47TH CLASS VII GRADUATION CEREMONY IRENTE SCHOOL FOR THE BLIND

Today, 20th September 2019 there was held the 47th class VII graduation ceremony after the inception of Irente School for the Blind in 1963. Eight students graduated. The Guest of Honor of the occasion was the North Eastern Diocese Bishop, who was represented by Rev. Paulo Diu, the Coordinator for Education in the Diocese. In his speech, Pastor Paulo Diu urged the community not to marginalize and look down on the children with multifaceted disabilities. Among the participants at the event were; Stephen Shemdoe (the Lushoto District Council Special Needs Education Officer), Glory Mdemu (the Lushoto District Council Community Welfare Officer), Rev. Happyness Diu (The Diocesan Gender and Children Coordinator), Heads of Irente Diaconal Institutions and head teachers from neighboring  primary schools. At the event, a minor fund raising for the development of school was done. Earlier before getting in venue of the ceremony the Guest of Honor with his delegation and other participants saw exhibitions that were performed by students and their teachers.