ELCT North Eastern Diocese
Mwendelezo wa Maadhimisho na Mafunzo ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia
- Details
Siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zinaendelea katika mikoa yote Tanzania, ambapo leo tarehe 04/12/2020 Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa kushirikiana na Kituo cha Watoto Wenye Ulemavu wa Akili (Irente Rainbow School) wametoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga.
ulimwengu ukiwa katika siku 16 za kuhamasisha kupinga ukatili wa kijinsia hususani kwa wanawake na watoto.Baadhi ya watu wenye mahitaji maalumu wilayani Lushoto Mkoani Tanga wameomba kuwekewa mazingira yenye uhakika wa kupata elimu bora, hali itakayo pelekea ushiriki wao kuwa mkubwa katika ngazi za maamuzi na uzalishaji mali.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye semina iliyo jumuisha wazazi na walezi wenye watoto wenye mahitaji maalumu iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa kushirikiana na Kituo cha Watoto Wenye Ulemavu wa Akili (Irente Rainbow School) wameiomba serikali na wadau wakati huu kuwawekea mazingira rafiki ya wao kupata elimu ya darasani na ya ujuzi wa kujitegemea.
- Hits: 1689
Ibada ya Kipaimara Usharika wa Handeni Jimbo la Tambarare
- Details
Leo tarehe 29/11/2020 imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa Handeni Jimbo la Tambarare Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMS) ambapo vijana wapatao 9 walipata kipaimara na mmoja kati yao alibatizwa.Ibada hiyo iliongozwa na Mch.William Karata na Mch.Ismail Ngoda.Ibada ilihudhuriwa na Wachungaji, Wainjilisti,Mashemasi,Kwaya,Washarika pamoja na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Usharika wa Handeni unao ongozwa na Mch Lewis F.Shemkala
- Hits: 2351
Mkutano Mkuu wa 3 baada ya miaka 125 ya Injili KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.
- Details
Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMS) imefanya Mkutano Mkuu wa 3 baada ya miaka 125 ya Injili ulioanza tarehe 25-26/11/2020 ikumbukwe mkutano huu ulikuwa na ajenda kuu moja ya Uchaguzi wa Askofu mpya wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na viongozi wengine.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati maalumu ya kuratibu shughuli za mkutano mkuu wa uchaguzi wa Askofu ni Askofu Mstaafu Dkt. Paulo Akyoo toka KKKT Dayosisi ya Meru ambaye baada ya uchaguzi alimtangaza Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu aliye chaguliwa na Wajumbe wa mkutano Mkuu kuwa Askofu mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa kupata kura 194 sawa na 89.4% .
- Hits: 3611
Page 7 of 28