ELCT North Eastern Diocese
Ibada ya Kipaimara Usharika wa Malibwi,Youths Confirmation at Malibwi Lutheran Parish
- Details
Mnamo tarehe 13/09/2020 imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa Malibwi Dinari ya Kaskazini.Ambapo ilifanyika ibada iliyokuwa na matukio mbalimbali vijana wapatao 135 walipata kipaimara 8 kati yao walibatizwa na ndoa moja ilibarikiwa.Liturgia katika ibada hiyo iliongozwa na Mch Benjamin Chambo mchungaji wa usharika na mzaidizi wa mkuu wa Dinari ya Kaskazini, na Mch Paulo Diu Mratibu wa Missioni na Uinjilisti alihubiri neno la Mungu.
- Hits: 337
Ibada ya Kipaimara Usharika wa Mlalo,Youths Confirmation at Mlalo Lutheran Parish
- Details
IBADA YA KIPAIMARA USHARIKA WA MLALO
Leo imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa Mlalo Dinari ya Kaskazini.Ambapo imefanyika ibada iliyokuwa na matukio mbalimbali vijana wapatao 118 wamepata kipaimara 8 kati yao walibatizwa na ndoa moja ilibarikiwa.Liturgia katika ibada hiyo iliongozwa na Mkuu wa Dinari ya Kaskazini Mch Peter Bendera, na msaidizi wa Baba Askofu Mch Dkt Eberhardt Ngugi alihubiri neno la Mungu. Awali ibada ilitanguliwa na uwekwaji wa jiwe la msingi katika nyumba ya mtumishi.
Msaidizi wa Askofu Mch Dr. Eberhardt Ngugi akimbatiza mmoja wa vijana waliopata kipaimara
Assistant to the Bishop Rev. Dr. Eberhardt Ngugi baptizing one of the Confirmands
- Hits: 2316
Ibada ya Kipaimara Usharika wa Shume Youths Confirmation at Shume Lutheran Parish
- Details
Leo tarehe 23/08/2020 imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa Shume Dinari ya Kaskazini, ambapo vijana wapatao 212 walibarikiwa.Liturgia katika ibada hiyo iliongozwa na Mkuu wa Dinari ya Kaskazini Mch Peter Bendera, na msaidizi wa Baba Askofu Mch Dkt Eberhardt Ngugi alihubiri neno la Mungu.
- Hits: 1811
Mradi wa kuimarisha maisha ya watoto na vijana wenye ulemavu katika Milima ya Usambara - katika kipindi cha Covid-19
- Details
Mradi wa kuimarisha maisha ya watoto na vijana wenye ulemavu katika Milima ya Usambara- katika kipindi cha Covid-19 yamefanyika mambo mbalimbali ikiwemo utoaji elimu juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa huu. Maeneo hayo ya mradi ni katika baadhi ya kata na vijiji wilayani ya Lushoto, Halmashauri ya Bumbuli na wilaya ya Mkinga. Hii ikiwa ni pamoja na ofisi za serikali za mitaa, mashuleni, nyumba za ibada (makanisani na misikitini).
- Hits: 4914
Page 10 of 28