ELCT North Eastern Diocese
Hitimisho la Semina elekezi kwa Wakuu wa vituo KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki
- Details
Kaimu katibu Mkuu Mch. Godfrey T. Walalaze leo tarehe 05/02/2021 amehitimisha Semina elekezi ya mafunzo ya kuimarisha Vituo vya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki iliyo anza jana Katika ukumbi wa mikutano Cathedral ambapo amegusia mambo mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kuzijua Kanuni, Sheria na Taratibu za Kazi.
- Hits: 1092
Idara ya Jinsia na Watoto KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,Yapata uongozi mpya
- Details
Idara ya Jinsia na Watoto KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki imepata uongozi mpya ambao umechaguliwa kuiongoza idara hiyo kwa miaka minne ijayo walio chaguliwa ni Bi. Christina Peter ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Idara, Bi. Mercy Mushi, Makamu Mwenyekiti, Bi. Miriam Mndeme, Mwandishi na Bi. Flora Luziga, Mhazini.
(KATIKA PICHA NI) Mratibu wa Idara ya Jinsia na Watoto KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Happyness Diu wa pili kulia akiwa na Viongozi wapya, Bi. Flora Luziga wa kwanza kushoto, Bi. Mercy Mushi wa pili kutoka kushoto, Bi. Christina Peter wa tatu toka kushoto (Mwenyekiti wa Idara) na Bi. Miriam Mndeme wa kwanza kulia.
Kwa niaba ya Uongozi huo mpya Mwenyekiti wa Idara Bi. Christina Peter amewashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa imani kubwa kwao na kuahidi kufanya kazi hiyo kwa maslahi mapana ya Dayosisi na Kanisa kwa Ujumla.
- Hits: 1250
Page 3 of 28